Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amempa masaa 20 Injinia wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA), Felex Mafinga, kuwasilisha taarifa ya ununuzi wa Matishali matatu badala
ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali.
Agizo hilo amelitoka mjini hapa
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza bandari ya Tanga, na kugundua matumizi ya
pesa ambayo ni tofauti na agizo la Serikali.
Amesema Serikali ilitoa pesa kwa
ununuzi wa matishali mawili yenye uwezo wa kufanya kazi masaa 24 na badala ya
Mamlaka ya Bandari ikanunua matishali matatu ambayo hayana uwezo na kuhimili
upakuzi wa shehena katika meli zinazotia nanga katika kina kirefu cha maji.
Amesema kufuatia kufanywa madudu
hayo amemtaka Injia wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Felex Mafinga kuwasilisha
taarifa ofisi ya Waziri Mkuu ndani ya masaa 20.
Kwa upande mwengine Waziri Mkuu
amewataka Mkuu wa Mkoa, Mwantumu Mahiza, na Kamanda wa Polisi , Mihayo
Msikhela, kuzidisha doria mwambao wa bahari ya Hindi ili kuzuia uingizaji
wa Sukari na mali za mgendo.
Alisem Tanga imekuwa kinara wa
upitishaji na ushushaji wa Sukari na mali za magendo hivyo kuwataka kuzidisha
doria maradufu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment