Mahali ilipo na muonekano wake wa sasa bastola ya dhahabu ya Muammar Gaddafi
Ni miaka minne imepita toka auwawe aliyekuwa Rais wa Libya kanali Muammar Gaddafi na vikundi vya waasi wa nchi hiyo, Gaddafi alikuwa
kiongozi ambaye ana miliki vitu vya thamani kubwa kama gari la kifahari
lakini alikuwa ana miliki Bastola iliyopambwa kwa dhahabu.
Bastola ya Gaddafi
baada ya kuuwawa kwake ndio ilitumika kama ishara ya ushindi kwa waasi,
ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wanatumia kuonesha hadharani kama
furaha ya ushindi wa kumuondoa Rais huyo madarakani, muandishi wa BBC Gabriel Gatehouse ambaye alikuwepo wakati wa mapinduzi ya Gaddafi, amerudi Libya kwenda kufanya stori kuhusu bastola ya dhahabu ya Gaddafi ilipo na kuhusu maisha ya waasi waliomuua Gaddafi.
Mjini Misrata, kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli, ndipo inapoaminika kuwa bastola hiyo ipo kwa sasa. Mohamed ndio aliokota bunduki hiyo karibu na mahali ambapo Gaddafi alikamatwa, na katika mtafaruku uliokuwepo, na pia alipoonekana na bastola hiyo, waasi wengine walidhani Mohammed ndiye aliyemuua Gaddafi, na papo hapo ndio akawa anatajwa kama shujaa wa mapinduzi nchini Libya.
Chanzo: BBC Swahili
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment