Stori tatu kubwa mtandaoni asubuhi ya February 3
Nimepitapita katika mitandao nimekutana
na stori tatu kubwa asubuhi ya February 3 zilizogonga headlines za
michezo. Mtu wangu wa nguvu Naomba nikusogezee stori tatu kubwa
zilizogonga headlines za soka February 3 hizi ni kutoka sokka.com
3- Baada ya jina la Pep Guardiola
kukaa kwenye headlines muda mrefu kuhusu timu gani ataifundisha msimu
wa 2016/2017, zilimalizika mwishoni mwa mwezi January, baada ya uongozi
wa Man City kuthibitisha kuwa takuwa kocha wao kuanzia msimu ujao, February 3 katika mitandao imegundulika kuwa Pep Guardiola atakuwa akulipwa pound million 21.
2- Klabu ya Guangzhou Evergrande ya China imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Atletico Madrid Jackson Martinez kwa rekodi ya usajili ya kihistoria kwa Ligi ya China pound milioni 31.8 . Martinez ambaye alijiunga na klabu ya Atletico Madrid mwaka jana ameshindwa kutamba ndani ya kikosi cha Diego Simeone.
1- Ikiwa zimepita siku kadhaa toka Pep Guardiola atangazwe kuwa atakuwa kocha wa Man City kuanzia msimu ujao, tayari anaripotiwa kuelekeza nguvu zake katika kutaka kumsajili kiungo wa Man United. Inaripotiwa kuwa Guardiola atakapotua Man City mwishoni mwa msimu Ander Herrera wa Man United ndio huenda akawa mchezaji wake wa kwanza kumsajili.
No comments:
Post a Comment