Mamlaka ya anga Zimbabwe yakamata ndege ya kimarekani, kwa kukutwa na maiti na fedha za Afrika Kusini
Mamlaka ya anga ya Serikali ya Zimbabwe
February 15 imetangaza kuikamata ndege ya kimarekani inayomilikiwa na
Western Global Airlines iliyokuwa imeomba kutua kwa dharura katika mji
mkuu wa Zimbabwe Harare. ndege hiyo iliyokuwa
inatoka Ujerumani ikiwa imebeba pesa za Afrika Kusini (rand) na maiti.
Ndege hiyo ya mizigo aina ya MD11
iliomba kutua kwa dharura Harare ili ipate msaada wa usalama, lakini
ilikuwa inaenda Afrika Kusini na ilitua Zimbabwe ili kuomba msaada wa
mafuta kabla ya kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini. Uchunguzi wa
ndege hiyo ulikuwa unaendelea.
Meneja wa mamlaka ya anga ya Zimbabwe
David Chaota amethibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo ya kampuni ya
Western Global Airlines, kampuni ambayo ipo Florida Marekani,
inaripotiwa kuwa ilianza kuomba kutua Msumbiji lakini ilikataliwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment