Tangakumekuchablog
Tanga, UMOJA wa
Wamiliki wa Vituo vya Mafuta Tanzania (TAPSOA) tawi la Tanga, limechagua
viongozi wake wapya baada wa awali kumaliza muda wake ikiwa ni kushughulikiwa
kero na haki za wamiliki wa vituo vya mafuta.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana
na kusimamiwa na Katibu Tapsoa Taifa, Tino Massawe, umemchagua, Said Baghozah
kuwa mwenyekiti, Amour Ali kutoka kampuni ya GBP kuwa Katibu na Shakir Twaibar
kuwa mweka hazina.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi
huo, Mwenyekiti mpya wa TAPSOA Tanga, Said Baghozah, alisema jambo la kwanza
ambalo atalifuatilia ni kuomba Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kupunguza
gharama za mashine ya mkononi ya DFD.
Alidai kuwa mashine hizo zinazouzwa
dola 2,500 ni bei ya juu hivyo baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wenye
zaidi ya kituo kimoja hawatamudu gharama za ununuzi hivyo kuiomba kupunguza ili
kila mmoja kuweza kununua.
“Mashine za mkono za utoaji risiti ni
zuri na lenye tija kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na Serikali, lakini bei iko
juu sana na itakuwa vigumu kwa watu wenye vituo zaidi ya kimoja” alisema
Baghozah na kuongeza
“Umoja huu nina imani kwanza
utawaweka kuwa kituo kimoja wamiliki wa vituo na kuwa na sauti moja katika
mambo mbalimbali, tuko na kero nyingi na malalamiko kwa Serikali na Mamlaka ya
mapato Tanzania” alisema
Kwa upande wake, Katibu wa umoja
huo, Amour Ali, alisema kwa kuchaguliwa kwake kuwa katibu wa TAPSOA tawi la
Tanga, wamiliki wa vituo vya mafuta watarajie kuona mabadiliko makubwa sekta ya
mafuta.
Alisema kero zote za wamiliki wa
vituo vya mafuta atazishughulikia pamoja na mambo mengine yakiwemo kushuka kwa
bei ya mafuta na kupanda ambayo imekuwa na misuguano ya mara kwa mara.
“Naomba ushirikiano wenu ili niweze
kutimiza yale yote ambayo nimepanga ikiwa ni maslahi kwetu wamiliki na wadau wa
mafuta kuanzia Serikali mnunuzi hadi kumfikia mlaji” alisema Amour
Alitoa pongezi kwa viongozi wa
Tapsoa Taifa kwa kuweza kushughulikia kero nyingi za wamiliki wa vituo vya
mafuta na kuwataka kuzidisha ushirikiano ili kuweza kuleta maendeleo na mageuzi
pamoja na mustakbali wa uchumi wa Taifa.
Mwisho
Katibu wa TAPSOA Taifa, Tino Massawe, akifungua kikao cha wamiliki na wauzaji wa mafuta mkutano uliofanyika jana Hoteli ya Tangabeach na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa mafuta ndani na nje ya nchi, Dubai, Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kufanyika Tanga
No comments:
Post a Comment