Tangakumekuchablog
Korogwe, SHULE ya
msingi Mbuyuni kijiji cha Toronto Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe Mkoani
Tanga, iko na walimu watatu na wanafunzi 33 baada ya wanafunzi wengi ambao ni watoto wa wafugaji
jamii ya kimasai kuyakimbia maeneo yao kutokana na migogoro ya ardhi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kitongoji, Mathayo Sangula, alisema
shule hiyo wanafunzi wengi wanaosoma
shuleni hapo ni jamii ya wafugaji.
Amesema kutokana na mgogoro wa ardhi
unaoendelea wafugaji wengi wameyahama maeneo
yao hivyo shule hiyo kubakiwa na walimu watatu na wanafunzi 33 na darasa
la tatu kufutwa baada ya kukosa
wanafunzi darasani.
Alisema darasa la saba liko na wanafunzi watatu ambao wanatarajiwa
kufanya mitihani yao ya taifa ya kuingia kidato cha pili wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya kuhakikisha wanamaliza silabasi
zote kabla ya mitihani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
kamati ya shule, Rajab Hassan, ameitaka Serikali kuinusuru shule hiyo kwa
kuondosha utengamano baina ya wafugaji na wakulima pamoja na wawekezaji.
Amesema shule hiyo iko na kero
nyingi ikiwemo maji na matundu ya vyoo
jambo ambalo limechangia kwa baadhi ya walimu kuacha kufundisha shuleni hapo.
Mwisho
Vijana wa Kimasai wakipita shule ya msingi ya Mbuyuni ambayo iko na walimu watatu na wanafunzi 33
No comments:
Post a Comment