Hofu ya kuachwa imesababisha amfanyie ukatili huu kwa mpenzi wake…
Mwanamke mmoja China, Azuha Kikuchi amekamatwa baada ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Yuji Hirata ambaye walikuwa wanaishi jengo moja kwa kumchoma kisu kifuani.
Polisi wamefanya uchunguzi na kugundua Kikuchi alimpiga mwanaume huyo kichwani na kumchoma na kisu kifuan ambapo mwili wake ulikutwa ndani ya chumba chake ukiwa na majeraha na walipomfikisha Hospitali alikuwa tayari amefariki.
Kikuchi alipohojiwa alikubali kuhusika na tukio hilo na kuwaambia Polisi kuwa kulitokea hali ya kutoelewana baada ya mpenzi wake kutaka kuvunja uhusiano wao.Ndani ya chumba hicho kulikutwa pia fimbo yenye wavu wa kuchezea tennis ukiwa na damu pamoja na kisu kilichokuwa kwenye begi ambavyo vilinunuliwa na Kikuchi siku chache kabla ya tukio hilo kutokea.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blospot.com
No comments:
Post a Comment