Azam Yarudi juu VPL.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara Azam Fc hii leo wamefanikiwa kurejea kwenye kilele cha ligi hiyo baada ya kuwafunga Mtibwa Sugar 5-2 katika mchezo uliopigwa huko Azam Complex Chamazi .
Azam walifunga mabao yao kupitia kwa mshambuliaji Kipre Tchete ambaye alifunga mabao mawili , Frank Domayo ambaye pia alifunga mawili , na Didier Kavumbagu huku Mtibwa wakifunga kupitia kwa Ali Shomari na Ame Ali .
Matokeo ya mchezo huu yamewafanya Azam Fc warudi kwenye kilele cha ligi hiyo wakiwa wamekusanya jumla ya pointi 25 ambapo wanawazidi Yanga kwa idadi kubwa ya mabao .
Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Mtibwa kupoteza huku ukiwa mchezo wa tatu kwa ujumla ambao wanafungwa tangu kuanza kwa Ligi ya msimu huu na mchezo huu pia unakuwa mchezo pekee ambao umeshuhudia idadi kubwa ya mabao ambapo jumla ya mabao saba yalitinga wavuni .
Huu ni mchezo wa mwisho kwa Azam kabla hawajaingia uwanjani kucheza na timu ya El Mereikh ya nchini Sudan katika mzunguko wa kwanza wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa jumapili ya wiki hii .
No comments:
Post a Comment