Hali ya hewa ilipochafuka wakati Rais Zuma akihutubia Bunge South Africa…
Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii
Duniani kote iko, ukiyaona leo Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona
hayo hata kwenye Mijengo ya Mabunge ya wenzetu yaani.
Jana kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini, mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma wakati
akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa
wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi
zinazomkabili.
“Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.
Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema
kutoka nje ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia
na kumtoa kwa nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge,
ambapo baadaye Rais Zuma aliendelea na hotuba yake.
Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment