
Mvutano
katika ishu ya utalii imeendelea kuingia kwenye headlines kubwa leo,
vyombo vya habari Kenya vimeripoti ishu ya Serikali ya Kenya kupiga
marufuku magari ya kitalii kutoka Tanzania kuingiza watalii katika mbuga
za wanyama na viwanja vya ndege vya nchi hiyo.
Waziri wa Masuala ya Jumuia ya Afrika na Utalii nchini humo,
Phyllis Kandie
ametangaza kutekelezwa kwa hatua hiyo mara moja hadi pale mzozo
uliyopo kati ya nchi hizi mbili juu ya masuala ya utalii
utakapomalizika.

Phyllis Kandie
Waziri huyo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mataifa haya
mawili kushindwa kufanya kikao maalum kama ilivyotegemewa baada ya muda
wa wiki tatu uliokuwa umepangwa kuisha.

Kwa
sasa magari ya watalii nchini Tanzania yataruhusiwa kuingia nchini humo
lakini yanatakiwa yawe na leseni, ingawa Kenya imeruhusu magari ya
watalii kuingia maeneo yote nchini humo, kwa upande wa Tanzania
imeruhusu magari ya kitalii kutoka Kenya kuingia katika mikoa ya Tanga,
Moshi, Arusha na Musoma.
Hutopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu niko tayari kukutumia kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment