Askari aliyeuawa akimuokoa mtoto Dodoma
Alhamisi ya February 05 ya leo inatokea Dodoma inahusu baba alijifungia ndani akimpiga mtoto wake wa miezi 8, mke wake alipomtaka afungue mlango alitishia kumuua.
Mama wa mtoto huyo alipoona hali
hiyo alikimbilia kituo cha Polisi ili kupata msaada, askari aliyefika
aliingia ndani ya chumba hicho kwa ili amuokoe mtoto huyo, baba huyo
alimkata kwa mapanga hadi kufariki.
Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa
Polisi huyo alifanikiwa kuingia kwenye chumba hicho na kumuokoa mtoto
huyo lakini wakati anatoka nje aliteleza na kuanguka ndipo baba huyo
alipopata nafasi ya kumshambulia kwa panga hadi kufariki.
Baada ya kusababisha mauaji hayo
mtuhumiwa alikimbia, Jeshi la Polisi wanamtafuta na taarifa kuhusu hali
ya mtoto huyo ni kwamba anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment