Jamaa aliyejulikana kama Edson amesema kuwa mume wake Pipi anaeitwa Lucas alienda na jamaa mmoja na kumuambia kuwa wanashida ya fedha ya kukomboa gari lao ambalo liko bandarini akawapa milioni tatu walizohitaji na kumuachia gari yao aina ya Toyota IST, badae alirudi akamwambia haikutosha na kuhitaji tena kiasi cha milioni mbili, ilipofika siku ya kurudisha fedha hizo alishangaa kuona gari inakamatwa.
Baadae msanii Pipi alipoulizwa kama anamjua Lucas ambae ni mume wake alikataa kuwa sio mume wake, ndipo walipotafuta vielelezo vikiwemo vyeti vya ndoa vilivyoonyesha kuwa ni mume wa msanii huyo.
No comments:
Post a Comment