Monday, February 9, 2015

MTOTO ALIEPATA ULEMAVU AWAPA FARAJA WAZAZI WAKE

Pale ambapo mtoto mwenye ulemavu wa miguu aliporudisha matumaini kwa familia yake

7427ea210acc163c1cf304Mtoto wa miaka minne ambae alikuwa kwenye hali mbaya baada ya kupata ajali  ya gari iliyopelekea kupoteza miguu yake yote miwili mwaka 2013 huenda familia ikasahau hata mzigo mkubwa wa deni la matibabu anayopatiwa katika Hospitali moja China kutokana na hiki alichokifanya.
Ukimuona hali yake inahuzunisha, lakini manesi, madaktari na ndugu walijikuta wakipata faraja ya aina yake kutokana na mtoto huyo kucheza wimbo huku akionekana kuwa na furaha mbali ya hali  alionayo.
Alijiachia akicheza wimbo wa ‘Little Apple‘ akiwa juu ya kitanda Hospitalini.
Baadhi ya watu waliyoiona video hiyo walishindwa kujizuia kutoa machozi pale walipoitazama, lakini wapo waliofurahia kumuona mtoto huyo akiwa mchangamfu na mwenye tabasamu muda wote.
Nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment