Saturday, February 14, 2015

MTOTO WA STAA CHINA AOMBA RADHI

Mtoto wa Jackie Chan leo kaongea na waandishi wa habari baada ya kutoka jela

001ec949f81b164952e41eJana nilikusogezea story ya kuachiliwa kwa mtoto wa actor Jackie Chan ambaye alikamatwa kwa kosa la kukutwa na bangi nyumbani kwake na pia kosa la kuruhusu watu wavute bangi nyumbani kwake.
Jaycee Chan ameongea na waandishi wa Habari na kuomba radhi kwa kosa hilo ambalo limemfanya akae jela kwa miezi sita.
Kama mtu ambaye ni staa kwenye jamii yake anaamini kwamba makosa yake yamemfanya aonekane mtu tofauti kwenye jamii yake.
Jackie Chan ni Balozi wa mapambano ya dawa za kulevya China tangu mwaka 2009, lakini hakuwahi kufanya ushawishi wowote ili mtoto wake aachiwe gerezani.
Watu wa China wanahisi Chan kaachiwa mapema kwa sababu baba yake ni mtu mwenye ukaribu mkubwa na viongozi wa juu wa Serikali ya nchi hiyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia m, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment