
Mwanamitindo
Flaviana Matata ambapo mratibu wake amezungumzia ishu ya ile kampeni iliyokuwa inafanywa na
Flaviana Matata Foundation ya
kuchangia vifaa vya kujenga Shule ya msingi Msinune iliyoko Bagamoyo,
amesema baadhi ya michango imeshakamilika na miezi michache ijayo
michango hiyo yakiwemo madawati vitakabiziwa kwenye Shule hiyo.

Baada
ya shindano la Miss Tanzania kufungiwa watu wengi wamekuwa wakijiuliza
endapo mshindi wa mwaka huu atashiriki katika mashindano ya Miss World
mwakani ambapo Miss Tanzania 2014,
Liliani Kamazima
amesema kuwa atashiriki kama kawaida ingawa hajui miaka miwili
iliyobaki na kuhusu kufungiwa kwa mashindano hayo amesema hatua hiyo
imeziba ndoto za wasichana waliotaka kushiriki.

mwanamziki
Q Chief alizungumzia ishu ya msanii
T.I.D kumlaumu kuwa yeye ndio chanzo cha
Top Bad kufa, na kukanusha vikali na kumtupia lawama T.I.D, leo msanii
T.I.D
amesema kuwa ameamua kutozungumza chochote juu ya jambo hilo na
kusikitishwa na maelezo ya Q Chief kwa kuwa alizungumza ukweli na kwa
sasa amenunua vyombo vingine na
Top Band iko pale pale.
No comments:
Post a Comment