Nimekuwekea Habari kutoka Kenya.
.
Watu wanne wanasadikiwa kuuawa baada ya wezi wa mifugo kuvamia eneo la Kainuke, Chifu wa eneo hilo Sara Lochodo amesema idadi kamili ya watu waliofariki bado haijajulikana na kusema wavamizi hao wanahisiwa kutoka jamii ya Wapokot.
Shirika la KWS limetoa
fidia kwa watu thelathini waliovamiwa na wanyamapori katika Kaunti ya
Marakwet, ikiwemo familia ya watu wawili waliofariki kwa kuvamiwa na
wanyama hao.
Serikali ya Kenya imetakiwa
kutowalazimisha walimu kurudi kazini katika maeneo ambayo wanahisi ni
hatari, Katibu Mkuu wa chama kinachotetea maslahi ya wazazi, Musau Ndunda amesema walimu hao wanapaswa kuhamishwa na sio kuwalazimisha warudi katika maeneo hayo.
Maafisa wa tume ya IBC
wamejikuta katika wakati mgumu baada ya wagombea wa uchaguzi mdogo wa
Seneta katika eneo hilo, kuanza kulaumiana hadharani kuhusu vurugu
zinazotokea wakati wa kampeni, hata hivyo mgombea wa chama cha ODM Moses Kajwang’ hakuhudhuria mkutano huo.
Tangakumekuchablog inakupatia habari kemkem kutoka kila pembe ya Dunia na usipittwe na uhodo huu mtu wangu.
No comments:
Post a Comment