Monday, March 2, 2015

AJIKATILI BAADA YA KUTAKIWA KUACHA KUCHEZA GAME

Ukatili aliojifanyia kijana huyu baada ya baba yake kumzuia kucheza TV Game..

who-knew-playstation-3-s-could-be-used-to-study-black-holes
Teknolojia imefanya vitu vingi kubadilika, zamani ilikuwa unakuta watoto wako mtaani wanacheza michezo kama kombolela, wanaruka kamba, siku hizi imegawanyika, kuna wale watoto wachache ambao wanacheza michezo hiyo, wengine siku hizi wanaangali movies, wanacheza games, wapo wazazi ambao hawaendi hii.
Mwanafunzi mmoja Hsueh Jun-Chen wa Taiwan amejiua kwa kujichoma moto baada baba yake kumzuia asicheze game ya TV na kumlazimisha kulala.
Chen alikuwa chumbani kwake, baba yake Liu aligonga mlango na kumlazimisha kijana huyo kulala
Siku iliyofuata baba yake aligundua mtoto wake hayupo kwenye chumba chake, akaenda garage akakuta pikipiki yake ipo lakini kulikuwa na madumu mawili ya petrol hayapo, akaanza kumtafuta ambapo aliikuta mwili wa mtoto ukiwa umeungua umbali wa kama mita 300 hivi toka kwenye nyumba yake na madumu hayo yapo pembeni yake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment