Monday, March 2, 2015

MAPACHA WAWA GUMZO KATIKA MITANDAO

Muonekano wa mapacha hawa umewafanya waingie kwenye Gumzo

twins

February 12 mwaka huu blog hii iliandika stori kuhusu watoto wawili mapacha kuzaliwa huku wakiwa wamepishana miezi miwili.
warembo2
Kwa mujibu wa wataalamu walisema watoto hao walizaliwa katika mifuko tofauti ya uzazi ambayo iliruhusu mmoja kuzaliwa kabla ya mwenzake.
wazazi
Lucy na Maria wakiwa na wazazi wao

Leo tena kuna stori inayowahusu wasichana hawa Lucy na Maria ambao ni mapacha kuingia kwenye headlines baada ya kutofanana kabisa na hadi kupelekea watu kuamini kuwa sio mapacha kutokana na muonekana wao ambapo mmoja anaonekana kuwa mweupe na mwingine mweusi.
wadogo
Lucy na Maria enzi za utoto wao

Kwa upande wa wazazi wao baba yao Vince ana asili ya mzungu na mama yao Donna ni raia wa Jamaica.
Lucy anaonekana ni mweupe kuanzia rangi ya ngozi hadi nywele huku Maria akiwa ni mweusi wa ranfi hadi nywele walizaliwa January 1997.
Hakuna anayeamini sisi ni mapacha.hata tukivaa sare hawaamini,hatuonekani kabisa kama mapacha na ilitubidi hata kwenda kuleta ushahidi wa vyeti vya kuzaliwa hospitali kuwahakikishia marafiki zetu”.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment