Story kutoka Ikulu TZ, kikao cha Rais Kikwete na viongozi wa chama cha albino..
Mzozo wa walemavu hao ulitokea eneo la
mapokezi ya Ikulu Dar ambapo wapo waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya
kuonana na Rais, lakini likajitokeza kundi jingine ambalo halikuwa
kwenye orodha hiyo, ilipofika muda wa kuingia ndani vurugu hizo zilianza
ambapo waliwazuia viongozi wasiingie ndani bila wao huku wakidai kwamba
kwa sasa hawana viongozi.
Tafrani hiyo iliendelea kwa muda na
kusabisha shughuli zote za mapokezi kusimama kutokana na kelele
zilizosababishwa na walemavu hao hali iliyosababisha Askari waliokuwa
eneo hilo kuingilia kati na kuwaambia watoke nje ya geti ili
wakajipange.
Mara baada ya kutolewa nje ya geti la
Ikulu walianza kurushiana maneno wao kwa wao huku wakimzomea Mwenyekiti
wao na kuzuia asihojiwe na waandishi wa habari waandishi wa habari muda
mfupi baadaye wakaanza vurugu ambapo maafisa wa usalama walifanikiwa
kumuokoa Mwenyekiti huyo.
Maafisa usalama wa Ikulu waliwaagiza
waondoke maeneo hayo lakini baadaye Mwenyekiti huyo aliwasiliana na
wenzake ambao walikuwa kwenye orodha ya kuingia Ikulu na kufanikiwa
kuongea na Rais Kikwete.
CHANZO: Habari ITV, March 5, 2015.
No comments:
Post a Comment