Pale ambapo ushirikina umehusishwa kwenye mauaji ya watu hawa mkoa wa Mara..
JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa Serikali ya kijiji cha Park
Nyigoti, wilaya ya Serengeti baada ya kutuhumiwa kuwakamata na
kuwafunga vitambaa usoni watu nane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha
kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.
Kaimu Kamanda wa Polisi na kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Ernest Kimola,
amesema tukio hilo limesababisha watu wengine watatu kujeruhiwa kwa
viboko na kulazwa katika Hospitali teule ya Nyerere DDH mjini
Mugumu, mbali na mwenyekiti na mtendaji viongozi wawili wa jadi
wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.
Wananchi hao walikamatwa katika miji
yao kisha kufunga vitambaa usoni na kuchapwa viboko hadi kufa kwa madai
ya kujihusisha na vitendo vya ushirikina, viongozi hao wa jadi kwa
kushirikiana na Serikali ya kijiji waliitisha mkutano kwa lengo la
kuwabaini watu wanajihusisha na ushirikina ambao umesabisha mvua
kutonyesha kijijini hapo ambapo watu wanane walitajwa katika
mkutano huo.
Kaimu Kamanda huyo amewasema tukio
hilo lililotokea alfajiri March 2 na kisha miili ya waliouawa ikitupwa
karibu nyumba zao huku watu wengine watatu wakilazwa Hospitali kutokana
na majeraha ya kupigwa.
CHANZO: Habari ITV March 05, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment