Utata wa taarifa ya msichana wa kazi kuingiliwa na baba mwenye nyumba
Malalamiko kuhusu baba mwenye nyumba
kushutumiwa kumbaka msichana wake wa kazi baada ya kumlaghai ndiyo ishu
ambayo imehusika kwenye mitandao ya kijamii leo.
Ishu hiyo imetokea Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo
majirani walitishia kuandamana kwa kuwa baba huyo anashutumiwa lakini
hakuna hatua yoyote ya kesheria iliyochukuliwa.
Majirani wamesema kuwa binti huyo
aliwafuata akiwa analia na kulalamika kuwa tumbo linamuuma kutokana na
baba huyo kumlaghai na kisha kumbaka, wakaamua kumpeleka Polisi ambako
walipewa PF3 na kumpeleka katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa.
Mwenyekiti wa eneo hilo amesema alipata
taarifa baada ya mke wa baba anayetuhumiwa kwenda Hospitali kumchukua
binti huyo lakini walimkatalia na kumtaka aende na barua kutoka ofisi za
Serikali.
Daktari aliyemfanyia uchunguzi amesema
hakuna dalili ya msichana huyo kuingiliwa, majirani hao wameamua
kumpeleka ofisi za ustawi wa jamii ili wafanye uchunguzi zaidi.
Mke wa mwanaume huyo amesema alipigiwa
simu na mpangaji mwenzake akimpa taarifa hizo lakini alipomuuliza mume
wake kama alikataa kufanya kitendo hicho.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia wakati wowowte kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment