Collection ya picha kutoka kwenye nyumba mbili za kisasa zilizonivutia zaidi leo, gorofa na ya chini.
Nimependa
sana muonekano wa hii nyumba wakati wa usiku na hiyo mizunguko kuanzia
gorofa ya kwanza, imejengwa vizuri kama nyumba ya kuishi na sio kama
muonekano wa shule ya sekondari.
Leo nimepata hizi nikasema niwawekee watu wangu hapa, najua kuna ambao wanajenga, kuna ambao wameshajenga tayari lakini wanaweza kurekebisha na kuna ambao hawajajenga ambao uzuri wa nyumba kama hizi unaweza kuwapa nguvu zaidi ya kupambana na maisha au kuwapa idea kwenye kile kidogo walichonacho.
Hata kama hutojenga au hauna uwezo wa kuwa na nyumba kama hii, imani yangu ni kwamba ukitazama hizi picha unaweza kuokota chochote kama idea na ukaihamishia kwako.
Siku
zote vitu simple huwa vinanivutia sana, hii nyumba haina urembo mwingi
lakini imejitosheleza na inavutia, ukiangalia pembeni ya garden hakuna
matofali au mawe yaliyochorwa Zebra na bado muonekano ni mzuri sana.
Kitu
nilichopenda kwenye hiki chumba ni hiyo sehemu ya kuhifadhia nguo,
tumezoea makabati lakini hata huu mpango wa hivi ni mzuri kama chumba
kina nafasi.
No comments:
Post a Comment