
Hawa
watu ni kiboko na dunia imeendelea kuwaelewa kila siku zinavyosogea
yani, nilikua sijui kama HUAWEI iliingia kwenye bidhaa bora 100 za dunia
mwaka 2014 tena ikiwa bidhaa pekee ya China kuingia kwenye hiyo top
100.
Maonyesho ya
bidhaa za simu duniani ambapo HUAWEI pia wanashiriki, nimekutana na
mapya mazuri wakati bado maonyesho haya yanaendelea ndio maana nikasema
nikushirikishe na wewe mtu wangu yasikupite haya mazuri kutoka HUAWEI.

Kama ulikua hujui
HUAWEI
ni kampuni inayoongoza katika teknolojia ya mawasiliano (ICT) duniani
ambapo kwenye hivi vitu vipya walivyovitambulisha March 1 2015 ni
Huawei MediaPad X2,
TalkBand B2,
TalkBand N1, pamoja na
LTE CarFi vinatumia teknolojia ya kisasa zaidi kuruhusu watumiaji wake kuunganishwa popote walipo.

Imagine sasa hivi wamekusogezea mpaka hii LTE CarFi, Internet mpaka kwenye gari
Katika kile ambacho dunia nzima inashangaa, Huawei wamezidi kurahisisha maisha kwa kuzindua
CarFi 4G LTE. Hivi ni vifaa ambavyo vina kasi hadi
150 Mbps
na vitaigeuza gari yako kuwa ‘hotspot’ ya kutawanya internet na
kuunganisha vifaa hadi kumi kwa wakati mmoja ambapo hapa Hispania,
Huawei wameweka vifaa hivi kwenye
magari 400 na vimeonyesha kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu kabisa.
Nakumbuka wakati vinatambulishwa vipya mkurugenzi mtendaji wa Huawei Consumer Business Group Richard Yu amesema “
kufuatia
mafanikio ya Huawei MediaPad X1 na kurithi muundo wa kipekee wenye kioo
kikubwa zaidi, MediaPad X2 inadhihirisha imani na utekelezaji wa ahadi
yetu katika kutengeneza vifaa vyenye ubora wa hali ya juu tukitumia
teknolojia na uvumbuzi wetu mpya”

Huawei MediaPad ni ya kipekee sana kwani ni Phablet (phone+tablet)
yenye 8 Core, kioo
HD na wembamba , yenye kutumia laini mbili na hivyo kuifanya kuwa
simu ya kwanza duniani ikiwa na teknolojia ya LTE.
Yu akasema tena “
Ikiwa ni aina ya pili
ya MediaPad, Huawei MediaPad imejikita kwenye matumizi matano yenye
umuhimu zaidi kwa watumiaji. Matumizi hayo ni pamoja na ubora wa simu
zinazopigwa, application za mitandao ya kijamii, manunuzi mtandaoni,
video na picha zenye kuongeza tija kwa mtumiaji, tuna imani kuwa
MediaPad itaendelea kuongeza ari kwa watumiaji kupitia muundo wake wa
kipekee na uwezo wake wa hali ya juu.”

Unaambiwa
Huawei ni kampuni namba moja ya teknolojia ya mawasiliano (ICT) duniani, ikiwa na makao makuu yake huko
Shenzhen China, wana maabara na vituo 16 vya utafiti wa teknolojia mpya kwenye nchi mbalimbali duniani ikiwamo
Ujerumani, Sweden, Marekani, Ufaransa, Italia, Urusi, India na China.

Kwa
upande wa Talkband B1, hivi ni vifaa vipya ambavyo huvaliwa mkononi
vikiwa ni muunganiko wa ‘headset’ na uwezo wa kupima shughuli za mwili
kama vile mazoez, pia Huawei wamezindua
Talkband N2 ambazo hufanya kazi sawa na
Talkband B1 isipokuwa huwa na sauti zenye ubora zaidi kwa wale wapenzi wa muziki waliodata na muziki.

Vifaa
vya Huawei hutumika na moja ya tatu ya watu wote duniani kwenye nchi
zaidi ya 170. Mwaka 2014, Huawei ilikuwa ni kampuni ya tatu kwa
uzalishaji na usambazaji wa ‘smartphones’ duniani.

Kama unahitaji maelezo zaidi unaweza kutembelea:
consumer.huawei.com
No comments:
Post a Comment