Friday, March 13, 2015

KAMPUNI YA USAFIRISHAJI ABIRIA, FREYS COACH YAANZISHA ROUT TANGA HADI SINGIDA KWA LUXURY BUS

Tanga, KAMPUNI ya usafirishaji abiria, FREYS COACH, imeanzisha safari zake kutoka Tanga, Moshi hadi Singida kwa mabasi yake mapya (LUXURY BUS) ambayo mbali ya huduma zake za vinywaji, vitafunwa  na viburudisho pia mteja anaweza kukata tikiti yake kwa njia ya mtandao.
Mapinduzi haya mapya katika sekta ya usafirishaji abiria imepokelewa kwa mikono miwili na watu mbalimbali na kuishauri pia kuweka njia tofauti ili kuweza kupata huduma kama hizo kwa Mikoa mengine.
Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa usafiri huo, Kaimu Mkurugenzi wa Freys Coach, Hanfrey Skauki, amewataka wakazi wa Tanga, Moshi, Arusha na maeneo mengine kuwa kampuni hiyo imedhamiria kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji abiria.
Alisema usafiri huo ambao utaanza rasmi kesho asubuhi kwa wakazi wa Tanga na Mkoa wa Arusha kwa magari hayo kupishana na kudai kuwa huduma zote za kiutu zinapatikana wakati wote wa safari.
“Kampuni ya Freys imedhamiria kuleta mageuzi katika usafirishaji abiria kwa kuwaletea magari ya kisasa (luxury bus)-----tunawaomba abiria wa Mikoa yote kutuunga mkono siku zote” alisema Hanfrey
Akifafanua zaidi juu usafiri huo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema ofisi zake kwa Tanga ziko barabara ya 12 mkabala na kituo cha mafuta au stendi ya zamani na kwa upande wa Moshi huduma zinapatikana ofisi zilizopo kituo huko.
Alisema kwa huduma za kukata tikiti kwa kwa wateja wa mbali na ofisi hizo wanaweza kutuma kwa njia ya mtandao wa simu , 0674 124723 bila kujali eneo na Mkoa aliko.
Akitoa shukrani zake mara baada ya taarifa hiyo, Mkazi wa Mikanjuni, Shembilu  Chambega, alisema ujio wa magari hayo itakuwa mapinduzi makubwa kwani  kwa miaka mingi walikuwa wakisafiri kwa kutumia magari ambayo hukumbana na kero nyingi zikiwemo joto kali ndani ya gari na kuseganasegana.(Msegomsego)
Akitoa ushauri wake aliitaka kampuni hiyo mbali ya huduma nzuri ambazo wanatoa wakati wa safari mwanzo hadi mwisho kukumbuka kuanzisha pia safari za Dar es Salaam.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa simu 0674 124723, 0655 157163 au 0655 9029292 ofisini
  Mwisho

 










No comments:

Post a Comment