Labda hii ni mpya kwako.. mbwa anayetembea na kuvaa kama binadamu.
Mbwa kwenye pozi zake na mavazi kama tu
binadamu, pata picha unakutana naye barabarani halafu anatembea tu kama
binadamu kwa miguu miwili.
Wachina hawajashindwa kitu, hii imezua
mjadala katika mitandao.. waliobahatika kukutana naye barabarani
walijikuta wakigeua vichwa kumcheki, imetokea China.
Mbwa huyo amevalishwa kofia, shati na
sketi, mgongoni amebeba begi kama mwanafunzi wa shule, halafu anakatisha
zake mtaani poa kabisa yani.
Zhu
anasema alianza kufundisha mbwa kama njia ya kujifurahisha miaka
20 iliyopita, baada ya kuona mafanikio aliona aendelee kufanya hivyo kwa
kuwafundisha mbwa wengine wengi.
Hapa chini video ya mbwa mwingine aliyejulikana kama Jemma anaetembea kama mtu mwaka 2013.
Hakuna Stori itakayokupita ,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment