Thursday, March 12, 2015

ZIMBWABWE YAFUNGIWA KOMBE LA DUNIA

Maamuzi ya FIFA kwa Zimbabwe kuhusu Michuano ya Kombe la Dunia 2018

fifa_1742811c
Mechi za kufuzu kwa michuano hiyo kwaupande wa nchi za Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi October mwaka huu, Zimbabwe ni moja ya nchi za Afrika ambazo hazijawahi kufuzu kucheza mechi za Kombe la Dunia.
Taarifa kutoka FIFA jana  inahusu uamuzi uliotolewa kwamba Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki katika mechi za kufuzu kombe la dunia kwa mwaka 2018, baada ya kuwepo kwa taarifa za nchi hiyo kukataa kumlipa kocha wake wa zamani, Jose Claudinei Georgini.
warrios-fans-v-liberia-550
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka Duniani FIFA imesema kuwa, imechukua hatua hiyo baada ya nchi hilo kushindwa kumlipa kocha huyo na kuongezea kuwa shirikisho la soka Zimbabwe, ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo mbali ya kwamba walipewa muda wa kutosha ili kufanya malipo hayo.
Zimbabwe
Hakuna Stori itakayokupita ,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment