Friday, March 6, 2015

MDAHALOKATIBA PENDEKEZWA WAFANA TANGA

Mdahalo huo  ambao ulikuwa wa kusisimua na kuwavutia watu waliohudhuria ulikuwa ukionyweshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Tanga Tv na wengi wao wameiunga mkono na kuwataka wananchi kuipokea.
Katika mdahalo kulikuwa na vionjo vya hoja za kisheria ambapo wengi walikuwa wanajiuliza kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa somo la sheria kituo hapo baada ya kila mmoja kutoa hoja za kisheria juu ya Katiba Pendekezwa.
“Toka mchakato wa kuandikwa Katika Mpya, Rasimu na sasa Katiba Pendekezwa wananchi walikuwa wakishiriki kwa hali na mali ili tu kuweza kupata Katiba iliyo bora---kuelekea Katiba Pendekezwa  makundi yote yatashirikishwa kama ilivyokuwa hapo nyuma? Na kama sio hivyo Katika itakayokuja itakuwa ni ile inayotakiwa na wananchi” aliuliza Lusekelo Emeiy
Emeiy aliwataka wananchi kuipitia Katiba Pendekezwa kifungu kimoja baada ya chengine na kuweza kutoa michango yao kutoka moyoni na kuacha kusemea pembeni na kupoteza haki zao kikatiba.
Kwa upende wake,  Mwanafunzi Sakina Mshangama,  ametaka Tume ya Mabadiliko  Katiba Mpya kuisambaza Katika Pendekezwa na wananchi kuweza kuipitia ili kuweza kutumika katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema Watanzania wengi wangependa kuona wanaingia katika uchaguzi mkuu wakiwa na Katiba Mpya ambayo pia  itawapa nafasi wagombea nafasi mbalimbali  za kuongoza kuipitia.
“Binafsi na watanzania wengi tungependa kuona tunaingia uchaguzi mkuu tukiwa na Katiba Mpya----hii pia itawapa fursa wa nafasi za kugombea kuipitia na kujua miongozo yao” alisema Mshangama
Kutokana na kivutio cha Mdahalo huo kunoga, watazamaji wa Televisheni na waliohudhuria waliomba kufanyika tena mdahalo mwengine kwani mbali ya kufaidika kwa mambo ambayo walikuwa hawayajui lakini pia umeibua Changamoto, Vuguvuvu, Hamasa , Utayari wa kuipokea Katiba Pendekezwa na Katiba yenyewe.
Mwisho



Mwanafuzi wa kituo cha Elimu cha New Age Centre Tanga, Lussekelo Emeiy akizungumza katika mdahalo wa katiba ya Katiba Pendekezwa uliofanyika Tanga.


 Mwanafunzi wa kituo cha Elimu cha New Age, Sakina Mshangama akizungumza katika mdahalo wa katiba Pendekezwa uliofanyika Tanga.








 Wanafunzi wa kituo cha Elimu cha New Age Tanga, wakifuatilia mdahalo wa Katiba Pendekezwa uliofanyika Tanga


 Tunafuatilia kwa makini, ndivyo wanavyoonekana wanafunzi wa kituo cha Elimu cha New Age Tanga.


No comments:

Post a Comment