Stori zenye nafasi kubwa MAGAZETINI TZ March 7, ziko hizi SABA- ‘Padri Feki’, ESCROW, Rais JK…
NIPASHE
Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato TRA, Loicy Appollo
anayedaiwa kupokea Tshs. Mil 80.8/- katika sakata la ESCROW jana
amegoma kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwa madai ya
kuwepo kwa zuio la Mahakama Kuu ambapo anafanya idadi ya waliogoma
kufikia watatu.
Wengine waliotangulia kugoma kuhojiwa na Baraza hilo ni Mbunge Andrew Chenge na Afisa Mtendaji wa RITA, Philipo Saliboko.
Appollo analalamikiwa kwa kupokea mgawo huo wa fedha kutoka kwa Rugemalila ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering ambayo ina mahusiano na TRA kama mlipakodi.
NIPASHE
Mafuta feki ya kula aina ya Oki na
Premier Gold madumu 300 yenye ujazo wa lita 20 ambayo yalikamatwa
Bandari bubu Bagamoyo yanatarajiwa kurudishwa Malaysia chini ya uongozi
wa Shirika la Viwango TBS.
TBS iliyazuia mafuta hayo kungia sokoni
mpaka yakapokaguliwa katika maabara ambapo chanzo cha gazeti la NIPASHE
kimesema mafuta hayo yalikutwa hayana ubora na mwagizaji wa mafuta hayo
alipewa taarifa kuyarudisha yalikotoka chini ya usimamizi wa TBS.
Chanzo hicho kimesema mzalishaji
aliyepewa kibali kuzalisha mafuta hayo nchoni anayatengeneza kwa
kiwangokinachotakiwa lakini haya yaliyoingizwa kwa njia ya panya
hayakuwa na kiwango kinachotakiwa ikiwemo kutokuwa na tarehe ya
kutengezwa na mwisho wa matumizi.
TANZANIA DAIMA
Jeshi la Polisi Morogoro linamshikilia Josephat Asenga
kwa kujifanya padre wa Kanisa Katoliki Jimbo la New York Marekani
ambaye alifikia parokiani hapo Mei mwaka jana na kujitambulisha kwa
viongozi wa kanisa la Modeko kuwa amekuja kwa ajili ya mapumziko na
kuomba kuendesha ibada kanisani hapo.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 5 katika Kanisa Katoliki la Modeko Jimbo la Morogoro akiwa na majoho saba ya upadri.
Padri huyo alionesha kitambulisho
kilichofanya wampe ruhusa kuendesha misa bila matatizo, baada ya
kumaliza misa walianza kumtilia shaka na kuanza kumfuatilia na kupata
taarifa kwamba alikuwa akiishi na mwanamke kinyume na sheria za kipadri
za kanisa hilo.
Baada ya kukamatwa alihojiwa na kukubali
kwamba ni kweli yeye sio padri, Polisi wanaendelea na uchunguzi japo
tayari taarifa za kutoka Makao Makuu ya Kanisa hilo wamethibitisha
kwamba Asenga sio padri wa Kanisa hilo.
TANZANIA DAIMA
Vijana waliohitimu Mafunzo ya JKT
wamemwomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP katika Mahakama ya Kisutu
awaondolee masharti ya dhamana ili waweze kutibiwa kwa kuwa baadhi yao
ni wagonjwa na wanakosa matibabu.
Maombi yao yaliwasilishwa jana baada ya
wakili wa Serikali kudai kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa
hivyo aliomba tarehe ya kuahirishwa ambapo Hakimu Moshi
alisema mshtakiwa ambaye ni mgonjwa anapaswa kumwandikia barua DPP ama
wenzake kuandika kwa niaba yake lakini pingamizi la dhamana lililowekwa
na DPP Mahakama haina mamlaka ya kutengua.
Mshtakiwa mwingine Jacob Mang’ita
amesema yeye sio miongoni mwa watuhumiwa ila alikamatwa alipokwenda
kumjulia hali mgonjwa wake katika Hospitali ya Muhimbili ambapo Hakimu Moshi alisema shauri hilo litatolewa wakati ambao itafikia hatua ya ushahidi.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete
amewataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuwajengea uwezo
waandishi wa habari kwa kuwapatia mafunzo kila mara, pamoja na kuboresha
maslahi yao kwani wakishindwa kuwalipa vizuri, waandishi hao watalipwa
na watu wa mtaani jambo ambalo linaweza kupunguza weledi.
Rais Kikwete ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua rasmi kituo cha Televisheni cha Azam kinachomilikiwa na Kampuni ya Said Salim Bhakresa (SSB)
huku akimmwagia sifa Mwanyekiti wa Kampuni hiyo Said Salim Bakresa kwa
kueleza kuwa uwekezaji alioufanya utaongeza ushindani katika sekta ya
habari na kukitaka chombo hicho kuweka mbele maslahi ya utaifa kama
wanavyofanya mashirika makubwa ya habari duniani kama vile BBC na CNN nao wanazingatia utaifa wao kwanza.
“Tanzania
ni moja ya nchi zilizofanya vizuri katika kuhama kutoka kwenye mfumo wa
habari wa analogia kwenda digiti kwa ubora wa hali ya juu hivyo
kuzinduliwa kwa Studio za Azam TV kutaendeleza kuongeza ufanisi wa ubora
wake,”Amesema Rais Kikwete.
Amesema sekta ya habari ni moja ya
mhimili mkubwa hapa nchini ambao kazi yake ni kuhakikisha kuwa suala la
Demokrasia linaendelea kukua na kuthaminiwa, hivyo Serikali itaendelea
kusimamia uhuru wa vyombo vya habari kwa kutunga sheria zisizo
kandamizi.
“Siku
zote penye bidii penye maarifa penye mipango ya uhakika hakuna
kisichowezekana, hawa jamaa wameanzia mbali sana bidiii imewafanya
wafikie mahali hapa walipo:- aliongeza, Tumezoe kula vitu vya Azam,
kunywa vitu vya Azam, kushabikia timu ya Azam na sasa tutasikiliza Azam,
hii ni kazi nzuri kwa taifa hili”– alipongeza Rais Kikwete“
MTANZANIA
Mpango wa ugawaji wa vyakula vya msaada
na vifaa vingine kwa waathirika 250 wa mafuriko Kahama uligeuka shubiri
baada ya Mwenyekiti wa CCM Shinyanga, Hamis Mgeja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Benson Mpesya kutaka kupigana mble ya Mkuu wa Mkoa, Ali Rufunga.
Mtafaruku huo ulizuka wakati viongozi hao walipoanza kushutumiana ambapo Mgeja alianza kumshambulia Mpesya akidai DC huyo ametoa kauli za kuwakejeli ambapo Mpesya akajibu kwamba hana kawaida ya kujibizana na Mwenyekiti wa Chama Mkoa.
Licha ya Taasisi kadhaa kutoa misaada
kwa waathirika hao wa mafuriko kumekuwa na malalamiko kwamba misaada
hiyo ya vitu ikiwemo mablanketi na magodoro imekuwa ikiuzwa, alipoulizwa
DC Mpesya amesema kuwa hana taarifa na suala hilo lakini kwa kuwa limemfikia basi atalifanyia kazi wakati wowote.
Ripoti ya Hospitali walikolazwa majeruhi
wa maafa hayo inaonesha kuwa mpaka sasa idadi ya majeruhi waliobaki ni
37 kati ya 100 waliofikishwa kutibiwa.
MTANZANIA
Kitendo cha watu wenye ulemavu wa ngozi
kupigana Ikulu kimezua gumzo sehemu mbalimbali ambapo tafrani hiyo
ilitokana na mvutano wa kugombea nafasi ya wawakilishi 18 waliotakiwa
kuonana na Rais Kikwete.
Ofisa Mawasiliano wa Chama cha Albino (TAS), Josephat Torner amesema kitendo cha wao kupigana Ikulu ni ishara ya uchungu dhidi ya wenzao wanaouawa kikatili.
Akizungumzia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho Torner
alisema unatokana na masuala ya Kikatiba ambapo wanachama walitaka
kufanyika uchaguzi mapema lakini Azimio la Mkutano Mkuu liliagiza
uchaguzi huo kufanyika mwezi Julai.
Torner aliipongeza Serikali kwa kuchukuliwa hatua ya kunyongwa kwa watu waliohusika na mauaji ya albino.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment