Tuesday, March 10, 2015

MKE WA LAURENT GBAGBO JELA MIAKA 20

Hukumu iliyotolewa na Mahakama Ivory Coast kwa mke wa aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo..

gbagbo-wife-Simone-Gbagbo
Mara nyingi watu huwa wanalalamika, wanasema viongozi na watu wenye pesa hata wakifanya makosa hawafungwi, lakini ikitokea mtu wa kawaida kafanya kosa lolote anahukumiwa kifungo, hapo ndio ambapo watu wanalalamikia kwamba inaonekana kama hakuna usawa kwenye Sheria.
Mahakama ya Ivory Coast imemhukumu Simone Gbagbo mke wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo kifungo cha miaka 20 gerezani.
Simone amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011  na kusababisha vifo vya  watu zaidi ya elfu tatu.
Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, Laurent Gbagbo ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu ICC iliyopo The Hague, Uholanzi kwa makosa hayo kutokana na machafuko yaliyotokea mwaka 2010 baada ya Rais huyo kugoma kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara aliyeshinda nafasi ya Urais kutoka chama cha upinzani.
Gabga
Laurent Gbagbo na mke wake Simone siku ambayo walikamatwa kwenye Hotel, Abidjan 2011

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment