
Info ya kwanza kusikika March 6, ni ishu ya bodyguard wa msanii
Diamond Platnumz anayefahamika kama
Mwarabu Suleimani
ambaye alikuwa Tajikistan kushiriki kwenye mashindano ya kupigana ya
mieleka ambayo yalikuwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Mwarabu
amesema mchezo wa kwanza alicheza na jamaa wa Italy na game ya pili
alicheza na jamaa kutoka Iran lakini matokeo hayakuwa mabaya tofauti na
alivyotegemea, siku mbili kabla ya pambano la mwisho alipata jeraha
mguuni wakati akifanya mazoezi na kupoteza michezo miwili.

Weekend hii msanii
TID kwa kushirikiana na Radar Entertainment pamoja na msanii
Nazizi kutoka Kenya watafanya show Club
Bilz, akizungumza kwenye 255
TID
amesema amejipanga vema kwa kuwa ni show yake ya kwanza mwaka huu na
kutakuwa na wasanii mabalimbali pamoja na surprise za kutosha pamoja na
uzinduzi wa video ya msanii
Masai Sharo.

Story
ya mwisho kusikika inahusu uzinduzi uliofanyika jana wa program mpya
chini ya msimamizi wa hakimiliki wa Afrika Mashariki (East African
Copyright Management) ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba.
Utaratibu mpya ambao utasimamiwa na program hiyo ni ishu ya wasanii kulipwa na vyombo vya habari vinavyocheza kazi zao, msanii Nikki Wa Pili ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria ambaye amesema itasaidia msanii kupata matunda ya kazi anayoifanya.
No comments:
Post a Comment