NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA DELTA YAPATA AJALI UWANJA WA NDEGE LAGUARDIA NEW YORK
Ndege ya shirika la ndege la Delta imepata
ajali ya kuteleza kwenye theluji ilipokua ikitua kwenye uwanja wa ndege
wa LaGuardia wa New York, ndege hiyo iliyokua ikitokea Atlanta iliacha
njia na kugonga uzio wa seng'enge ya waya kama inavyoonekana kwenye
picha na msemaji wa zima moto ameripoti hakuna mtu aliyekufa kwenye
ajali hiyo isipokua baadhi ya ya abiria wamepata majeraha ya kawaida na
walikimbizwa hospitali kwa matibabu na kwa sasa uwanja huo umefungwa kwa
ndege kuruka au kutua mpaka saa 1 usiku kwa saa za Amerika ya
mashariki.
Abiria wakisalimisha maisha yao baada ya ndege ya shirika la ndege la
Delta kupata ajali ilipoteleza kutoka kwenye njia yake kutokana na
theluji inayoendelea kuanguka mapema leo.
Abiria wakitoka kwenye ndege kuokoa maisha yao
No comments:
Post a Comment