Friday, March 13, 2015

RAIS WA KOREA KUSINI NAE HAKUWA NYUMA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Siku ya wanawake Duniani Rais wa Korea Kusini hakukosa zawadi ya kuwapa wanajeshi wanawake

Image: North Korean leader Kim Jong-un visits the Thrice Three-Revolution Red Flag Kamnamu Company under the Korean People's Army Unit 4302
Katika mataifa ambayo hayako kwenye uhusiano mzuri duniani ni Marekani na Korea Kusini, Kim Jong-Un ambaye ni Rais wa Korea Kusini amekuwa akitajwa kama mmoja ya viongozi ambao hawatabiriki kwenye suala la maamuzi, anaamua chochote atakachojisikia kwa wakati wowote.
Siku ya March 8 dunia nzima ilisherehekea siku ya wanawake Duniani, watu wakapeleka zawadi kwa dada zao, ndugu zao wa kike, lakini mlengwa mkubwa alikuwa mama.
Rais wa Korea nae alikuwa na zawadi kwa wanajeshi wake wanawake ambao wako kwenye Kambi ya siri ya Jeshi la nchi hiyo, katika ziara  yake hiyo amegawa vitu kadhaa kwa wanajeshi hao ikiwemo vipodozi vya wanawake kama vile poda na vingine.
Japo Kim hakukutana na wanajeshi hao mmoja mmoja lakini mzigo wa zawadi hizo ulifikishwa kwa Mkuu wa Kambi hiyo na kuagizwa kwamba ni zawadi ambazo zinatakiwa kumfikia kila mwanamke ambaye yuke kwenye kambi hiyo.
Wewe ulimpa zawadi gani mama yako? Unaweza kuniandikia yako hapa lakini Rais Kim yeye katoa zake vipodozi.

No comments:

Post a Comment