Rais huyu ametajwa na kupewa TUZO yake ya Rais BORA Afrika…
Tumesikia story nyingi kwenye vyombo vya
habari vya Kimataifa, nyingi zaidi utasikia kwenye ishu kama kama
ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na mengine, ni mara
chache kukutana na stori za viongozi wakizungumziwa kwa mazuri.
Rais wa Namibia anayemaliza muda wake, Hifikepunye Pohamba ameshinda tuzo yenye thamani kubwa ya Mo Ibrahim inayotolewa kwa viongozi wa bara la Afrika.
Tuzo hiyo ina thamani ya dola milioni 5
na hutolewa kila mwaka kwa kiongozi wa nchi ambaye ameshika madaraka
kwa kuchaguliwa na wananchi na aliyeongoza vizuri nchi yake pamoja na
kuboresha maisha ya wananchi akiwa madarakani kisha kuondoka madarakani.
Rais Pohamba anakaribia kutoka madarakani baada ya kuiongoza Namibia kwa awamu mbili.
Mfanyabiashara raia wa Sudan, Mo Ibrahim ndiye mwanzilishi wa Tuzo hiyo na aliianzisha kwa ajili ya kuwapa motisha viongozi wa Afrika.
Zawadi hiyo ya dola mil. tano
inatolewa kwa kipindi cha miaka kumi kwa mshindi wa Tuzo hiyo, halafu
baada ya hapo atakuwa anapewa dola laki 2 kila mwaka mpaka mwisho wa
maisha yake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment