Monday, March 9, 2015

TAARIFA NYENGINE USHAHIDI KESI YA RUTO

Taarifa nyingine kuhusu shahidi wa Makamu wa Rais Kenya kwenye kesi ya ICC

Ruto
Makau wa Rais Kenya, William Ruto ndani ya Mahakama ya ICC.
Serikali ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa mtu mmoja uliopatikana katika mbuga ya wanyama ya Tsavo, kuwa ni wa Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya William Ruto. kwenye Mahakama ya ICC.
Mkemia wa serikali ya Kenya ametangaza kuwa mwili huo ambao ulikuwa umehifadhiwa  kwenye chumba cha maiti tangu mwezi December mwaka 2014 ni wa Meshack baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA.
_80131099_photo4
Meshack Yebei
Meshack Yebei alitekwa mwishoni mwa mwezi December nyumbani kwake Eldoret alipokwenda kumwona mkewe aliyekuwa anaumwa, familia yake ililalamika kuwa kutoweka kwa Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo.
Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye kesi yake ya mauaji inayoendelea Mahakama ya ICC, The Hague.
Marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa, Serikali ya Kenya itafanya uchunguzi kugundua kilichosababisha kifo chake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment