
Picha ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha muigizaji wa Bongo Movie,
Chopa Mchopanga
akiwa amevalia jezi ya timu ya Yanga, mkononi ameshika vidonge vingi na
chupa ya bia, watu walipoona hiyo wakaandika kwamba jamaa anataka
kujiua kutokana na timu yake kutofanya vizuri.
Mwandishi alimtafuta
Mchopanga
ambaye amesema hiyo picha ilitolewa kutoka kwenye movie mpya
itakayotoka hivi karibuni, sio kweli kwamba ana machungu na timu yake
kufungwa.
Jamaa amesema kuwa ana mapenzi na timu ya Yanga lakini kufanya vibaya
kwa timu hiyo hakumfanyi afanye uamuzi wa kujiua kwa kiasi hicho japo ni
kweli ana mapenzi nayo.
Hakuna Stori itakayokupita ,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment