Tanga, KATIBU
Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
Taifa, Silver Kiondo amekilalamikia kitendo cha Maofisa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga kutoka katika kikao cha Wafanyabiashara na kusema
kitendo hicho kunamaanisha hakuna ushirikiano.
Hapo jana, kimefanyika kikao cha
wafanyabiashara wenye maduka kujadili ongezeko la asilimia mia ya mapato pamoja
na matumizi ya mashine ya kutolea risiti na hivyo kushindwa kujadili baada ya
maofisa hao kutoka nje.
Akilizungumzia kitendo hicho, Katibu
huyo amesema wafanyabiashara wataendelea kuiomba Serikali kuangalia upya
ongezeko hilo sambamba na matumizi ya mashine vyenginevyo migomo ya nchi nzima
itafanyika.
Akizungumzia Kikosi cha Uokozi cha
Jeshi la Zimamoto kupita madukani na kukusanya kodi , amesema kitendo hicho ni
hatari kwani kikosi hicho ni sawa na jeshi na hivyo wanaweza kutumia nguvu za
kijeshi ili kujikusanyia pesa jwa nguvu.
Amesema kulazimishwa wafanyabiashara
kuweka kifaa cha kuzimia moto madukani ni cha uonevu na hivyo kuitaka Serikali
kufuta sheria hiyo kwani ni kuwanyonyoa wafanyabiashara kiuchumi.
"Kitendo cha Serikali kuruhusu kikosi cha Zimamoto na Uokozi kukusanya kodi za fere madukani ni hatari kwa usalama wa mfanyabiashara -----lile ni jeshi na watatumia mbinu za kijeshi kuhakikisha wanakusanya kodi " alisema Kiondo
Alisema kwa sasa Serikali inaonekana haina huruma kwa mfanyabiashara na wanataka kumkamua kila ambapo inaona ananufaika na hivyo kuitaka kulegeza masharti ili kuweza kufanya biashara na kuweza kulipa kodi bila mikwaruzo na maofisa TRA.
No comments:
Post a Comment