Ndoa ya Babu na Bibi nayo iko kwenye GUMZO
Tumezoea kuona vijana au watu wa makamo
kufunga ndoa lakini ilikuwa ajabu kwa vikongwe hawa kuchukua uamuzi huo
wakiwa na umri mkubwa.
Vikongwe hao Elder Dikam mwenye umri wa miaka 107 na Kala Nafung
mwenye miaka 95 kutoka nchini Nigeria wamemua kufunga pingu za maisha
huku wakiwashangaza watu kwa uamuzi wao huo kutokanana umri wao.
Imeelezwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa
kutokana na kila mmoja mwenza wake kufariki dunia na kuwaacha wapekwe
hivyo kuamua kutafuta faraja na kukutana kisha kuamua kufunga ndoa.
Bibi harusi ana mtoto wa umri wa miaka 65 ambaye ndiye pekee aliyebakia baada ya wengine kufariki.
Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Christ in Nations (COCIN) ambapo waliteka watu wengi waliofurika kushuhudia ndoa hiyo huku wakiwapongeza kwa hatua hiyo
Akisimulia historia ya maisha yake bwana
harusi alisema awali alikuwa na wake saba na watoto 32 enzi za ujana
wake na wakati huo alikuwa hamtambui Mungu na alikuwa na maisha ya kuoa
na kuacha kila wakati.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment