Wanne wahukumiwa kunyongwa kwa kuua albino
Watuhumiwa
wa kesi ya mauaji ya mlemavu wa ngozi, Zawadi Magimbu (32) wakiwa ndani
ya Mahakama Kuu Kanda ya Geita baada ya kuhukumiwa kunyongwa. Kutoka
kushoto ni Nasoro Charles, Singu Siantemi, Masaru Kahindi na Ndahanya
Lumola.
Watu
wanne wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na kosa la
kumuua Zawadi Magindu (32) mwenye ulemavu wa ngozi, mkazi wa Kijiji cha
Nyamaruru, Wilaya ya Geita mkoani hapa.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Jaji Joacquine De-Mello wa Mahakama Kuu, ambaye alisema Mahakama imeridhika pasi na shaka na ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka kwamba walihusika moja kwa moja na kifo hicho.
Waliohukumiwa
kunyongwa hadi kufa ni Nassoro Charles mkazi wa Kijiji cha Beda mkoani
Kagera, Masaru Kahindi mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru, Ndahanya Lumola na
Singu Nsiantemi wakazi wa Kijiji cha Kakoyoyo, Wilaya ya Bukombe.
Jaji
De-Mello alisema washtakiwa walifanya kosa hilo Machi 11, 2008 saa 1:00
usiku nyumbani kwa akina Zawadi wakati wakipata chakula cha usiku,
walimkata kwa shoka na panga miguu yote na mkono wa kulia.
Alisema
Masaru Kahindi aliyekuwa jirani na Zawadi, Nassoro Charles aliyekuwa
mume wa marehemu walivamia nyumbani kwao wakati wanapata chakula cha
usiku, huku wakiwa na panga na shoka kisha kumkata miguu na mkono wa
kulia .
"Watu hao
walikwenda na shoka na panga, walitumia shoka kumkata Zawadi huku mama
yake Magdalena Mashimba na mjukuu wake, Semen Hamisi wakipigwa na
kutupwa nje na wauaji hao," alisema Jaji De-Mello.
Aliendelea
kusema kuwa, wakati wanamkata Zawadi, mtoto wake Semeni alijibanza
mlangoni na kuwatambua wauaji hao kuwa mmojawapo alikuwa mume wa mama
yake na mwingine jirani yao.
"Waliona
na shahidi Magdalena na Semeni waliwatambua kwa sauti na mwonekano,
kwani wakati wanafanya hivyo kulikuwa na mwanga wa mbalamwezi," alisema.
Pia, Jaji
De-Mello alisema washtakiwa Ndahanya na Nsiantemi walikuwa
wafanyabiashara wa viungo vya albino, walikamatwa na polisi baada ya
kutegewa mtego.
"Polisi
walikuwa kwenye operesheni ya kuwatafuta watu wanaojihusisha na vitendo
vya kuua albino, walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna watu
wanataka viungo vya albino ndipo walipotafuta albino wawili, mmoja akiwa
mtoto na mwingine mtu mzima," alisema.
Alisema
baada ya kutegwa mtego huo walikamatwa washtakiwa wawili; Ndahanya na
Nsiantemi ambao walikiri kuhusika na mauaji ya Zawadi na kuchukua viungo
hivyo, kisha kuvipeleka kwa mganga wa jadi, Mussa Ally mkazi wa Katoro
ambaye alihusika kuvipima ili kujua iwapo vina ubora.
"Wakati
watu hawa wanahojiwa na polisi waliwataja wenzao wengi ambao hapa
mahakamani hawapo sijui ni kwa nini... wakiongozwa na Robert Kagoma
ambaye ndiye alikuwa wakala wa kulangua viungo hivyo na kuvipeleka kwa
mganga wa jadi aliyetajwa kwa jina la Gerald Mazuri ambaye pia huviuza
kwa 'wazungu' Geita," alisema Jaji De-Mello.
Hutpitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutmia wakati wowotew kupitia www.tamgakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment