Wednesday, March 11, 2015

WASEMAVYO KUTIMULIWA ZITTO KABWE CHADEMA

 Niseme kwamba kama kweli Chadema inataka kuleta mageuzi ya Kidemkrasia katika Uchagzu mkuu unaokuja imefanya uamuzi wa haraka kumfukuza ndani ya chama kwani ni kiungo muhimu na yuko na ushawishi mkubwa ndani na nje ya chama. Ushauri wangu ni vyema Zitto akabaki Chadema na suluhu ifanyike kwani kujiunga na vyama ni kuwagawa wananchi. Ali Juma Mkazi wa Manundu Korogwe Tanga.



 Hawakumtendea haki Zitto na uamuzi waliochukua ni wa haraka na inaweza kuwaletea doa Chadema  hasa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu. kwani Zitto yuko na ushawishi kwa vijana na wazee. Ushauri wangu kwa Zitto ni kuangalia upepo kwanza kwani Chama kikiyumba wanaweza kumkaribisha na kujiunga na harakati zao za mageuzi. Fredy Muya, mkazi wa Old Korogwe
Nashangazwa kuona Zitto amefukuzwa kwani najua kila chama cha siasa kinamtaka hata CCM, nisema wamempoteza mtu muhimu mwenye ushawishi ndani ya chama kwani kila alipokuwa anaenda alikuwa anavuna wanachama na watu walikuwa wanamsubiria. Ushauri wangu ni kwenda katika chama ambacho kitakuwa na mvuto wa mageuzi na kuweza kupata nafasi ya kuongoza na kuweza kututetea Bungeni hasa sisi vijana ambao hatuna ajira. Mtemi Juma mkazi wa Mtonga Korogwe

No comments:

Post a Comment