
Msanii
JI aliyewahi kufanya vizuri na single yake ya
‘Kidato Kimoja‘ lakini haikuchukua muda akahamia Kenya ambapo anafanyia shughuli zake mpaka sasa.
JI ambae
amesema kuwa alienda nchini humo kwa ajili ya kufanya show lakini badae
alipata dili la muda mrefu na kumfanya awe huko kwa muda wote huo,
kuhusu wimbo wake wa ‘
Kidato Kimoja’ amesema umemuingizia fedha nyingi na kumfanya aweze kubadilisha maisha yake na mpaka sasa bado unamuingizia fedha.

Msanii
Mr Blue amefunguka kuwa ngoma yake ya
‘Pesa’
imempa mafanikio makubwa ingawa hajaigharamia kitu chochote kutokana na
kupewa ofa na mshkaji wake kuanzia Audio hadi video, lakini
umemuingizia fedha nyingi na kumfanya aweze kumalizia ujenzi wa nyumba
yake pamoja na kununua gari jingine.

Weekend hii msanii
Diamond Platnumz ataonekana Live Afrika nzima akifanya show kwenye Tuzo kubwa za Film Barani Afrika, Meneja wake anaeitwa
Salam amesema show hiyo itafanyika Jumamosi ya March 7, ambapo itaonyeshwa Live katika Channel ya
Afrika Magic katika utoaji wa Tuzo za
Afrika Magic Movie Award ambazo zitafanyika Nigeria, msanii mwingine atakaefanya show ni
Iyanya ambae wanatarajia kufanya video ya wimbo waliofanya pamoja.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment