Ajali
Ni stori iliyoanza kuchukua nafasi kubwa sana katika mitandao mbalimbali usiku wa kuamkia October 16 2015 headlines za siasa Tanzania zimetawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).
Leo baada ya saa kadhaa, mgombea Ubunge kupitia CCM jimbo la Ukonga, Jerry Silaa alipost picha ya Helicopter na kuandika maneno kuhusiana na ajali hiyo>>>”Baba
yangu Capt.William Silaa akiwa na Mhe.Deo Filikunjombe na abiria
wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni
wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka
kwenye msitu wa Selous. Hakuna mawasiliano ya simu. Usiku kucha vyombo
vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na
jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii“ >>> Jerry Silaa.
‘Nawaomba
wote kuwa watulivu kwani jambo hili linahitaji umakini wa hali ya juu
na ushirikiano wa taasisi nyingi za wizara tofauti. Tuwaombee wote Mungu
awanusuru‘ – Jerry Silaa.
Baada ya hapo tukapata maelezo kutoka kwa Waziri wa Utalii na Maliasili, Lazaro Nyalandu akasema…>> “Tunaamini
kwamba Mungu atafanya miujiza juhudi za kuwapata nafikiri muda si mrefu
tunaweza tukafanikiwa, changamoto iliyosababisha watu wa msaada
kuchelewa kufika kwenye eneo la ajali moja taarifa za hiyo ajali
tulizipata wakati giza lilikuwa limeshaingia hilo la kwanza, la pili
ajali hiyo imetokea katika kitalu cha wawindaji kinachojulikana kama R3
na walioshuhudia walikuwa katika kitalu R2 tofauti yao ni kwamba
wametenganishwa na mto ambao unaenda kwa kasi halafu una mamba“>>> Waziri Nyalandu.
“Sisi
tulichokifanya kama Serikali ni kwamba tumetuma kikosi kimoja ambacho
kilikuwa kina askari nane.. Mkuu wa Polisi Mkoa wa Morogoro pia naye
akatuma askari kwenda kwenye eneo hilo la ajali, kwa hiyo lazima
tufahamu kwanza helikopta ilipodondoka na tutambue kama kutakuwa na wale
ambao watakuwa wamenusurika au wako wapi na leo Asubuhi tumetuma
helikopta kuangalia kinachoendelea… Tunasubiri taarifa za huko
watakaporudi kwani sehemu ambayo walipo hakuna hata mawasiliano ya simu” >>> Waziri Lazaro Nyalandu.
“Taarifa
tulizozipata kutoka kwa mashuhuda wa eneo hilo kwa wawindaji mahiri
walipiga simu kwa njia ya Satelite na kusema kwamba wameona helikopta
moja imeaguka msitu wa Selous kwenye kitalu R3 mto Ruaha baada ya hapo
wakaona moto kwa hiyo sisi kama Serikali tunaendelea kufanya uchunguzi
wakina” – Lazaro Nyalandu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment