Kuna watu maarufu hawapendi kubadilisha nguo, Rais Obama yumo.. Kuna sababu?
Unaweza kumuona Rais
Barack Obama kwenye suti moja au ya aina moja kila wakati, hapendi kubadilisha?
Marehemu Boss wa
Apple Inc, Steve Jobs nae yumo kwenye list… ana sababu yoyote?
Mwingine ni jamaa
Boss wa Facebook,
Mark Zuckerberg… kila ukimuona ni kama anakuwa na T-shirt moja tu, unakumbuka alichokijibu alipoulizwa?
Leo nimepata sentensi zao wote watatu.
Mwaka 2012 Rais Barack Obama aliwahi kujibu sababu iliyomfanya mara nyingi aonekane kwenye suti za rangi na aina moja >> “Sipendi kuamua kuhusu nini nitakula au nini nitavaa… nina mambo mengi zaidi ya kuyafanyia maamuzi kuliko hayo“>>>
Marehemu Steve Jobs.. Huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kampuni ya Apple Inc ya
Marekani, yeye pia kwenye mavazi yake mara nyingi alionekana na masweta
ya rangi nyeusi. Sababu yake pia kuonekana hivyo inatajwa kuwa ni
ileile ya uvivu wa kufanya maamuzi mapya ya nguo ya kuvaa kila wakati.
Mark Zuckerberg,
Boss wa Facebook nae anaonekana mara nyingi na T-Shirt ya Rangi ya
kijivu, ndio anayoipendelea zaidi na alipoulizwa alijibu >>> “Natakiwa nifanye maamuzi machache na ya msingi zaidi kwa ajili ya maisha yangu na kuisaidia jamii yangu“>>>
maana yake ni kwamba kwenye maamuzi yake, ishu ya kubadilisha nguo
haipo kwenye hesabu zake kabisa, Mark aliwahi kusema kwamba sio kwamba
habadilishi nguo ila anazo T-shirt nyingi za kijivu na ndio alizoamua
kuzivaa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment