Tuesday, October 13, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Mwanamke Msomali aliebakwa awasili  Australia

Nauru
Mwanamke raia wa Somalia anayedaiwa kushika mimba baada ya kubakwa katika kisiwa cha Nauru amewasili Australia kutolewa mimba hiyo.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 23 alikuwa ameomba ahamishwe kutoka kisiwa hicho cha Nauru wiki kadha zilizopita.
Kisiwa hicho humilikiwa na Australia na kimekuwa kikitumiwa kuzuilia watu wanaotafuta hifadhi Australia kabla yao kupewa idhini.
Mahakama kuu nchini humo kwa sasa inachunguza uhalali wa vituo hivyo vya kuzuilia wahamiaji.
Maelfu ya watu walijiunga na maandamano mwishoni mwa wiki kuunga mkono wakimbizi hao na kushinikiza serikali kufunga vituo hivyo.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na mimba ya wiki 12, na anadai alibakwa na wanaume wakazi wa Nauru.
Ni haramu kutoa  mimba katika kisiwa hicho pamoja na mafundishi ya dini, ila tu maisha ya mama yanapokuwa hatarini. Ubakaji hauchukuliwi kuwa sababu tosha ya mtu kutaka kutoa mimba ambapo ni haramu.
Serikali ya Australia ilikuwa awali imekabiliwa na shinikizo za kuitaka iwaruhusu wanawake kuingia nchini humo kupokea huduma za matibabu.
Australia

.Watawala katika kisiwa hicho wanasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai ya mwanamke huyo kwamba alibakwa na wanaume wawili Nauru.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablo

No comments:

Post a Comment