Marekani imeitaka
Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya
Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.
Waziri wa
mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameutaka utawala
nchini Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi
hayo.
Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika
mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao
wawili wa NATO. Mapema kupitia kwa hotuba yake, rais wa Uturuki
Recep Tayyip Erdogan alitoa wito kwa rais Obama kumrejesha nchini humo
kiongozi wa kidini raia wa Uturukli anayeishi nchini humo Fethullah
Gulen ambaye analaumiwa kwa kupanga mapinduzi hayo.
Bwana Gulen anayakana hayo. Marekani inasema kuwa Uturuki ni lazima ithibitishwa hayo kabla ya uamuzi wa kumrejesha Gulen kufanyika.
Mapema
nchini Uturuki maelfu ya watu walijitokeza wakiimba na kupeperusha
bendera ya taifa katika barabara za mji wa Istanbul na Ankara kumuunga
mkono rais Erdogan. Bustani nyingi mjini Istanbul zilijaa watu waliokuwa
wakiimba wakisema kuwa ardhi yao na demokrasia haviwezi kuchukuliwa na
jeshi.
Serikali imetawaka wafuasi wake kusalia katika bustani kuu
usiku kucha. Mashirika kadha ya ndege yalirejea safari zao kwenda
Istanbul Jumamosi jioni.
BBC
No comments:
Post a Comment