Thursday, February 12, 2015

INDONESIA NA MAPAMBANO NA MIMBA ZA UTOTONI

Tatizo la ujauzito kwa wanafunzi, Indonesia kuna ishu ya wanafunzi kupimwa bikira…

6ef9378d-5e3a-4984-8335-a59a049a0941-1020x612Ni zaidi ya mara tatu kumekuwa na mijadala ndani ya Bunge la Tanzania tumesikia ikijadilia kuhusu njia ambayo inasaidia kutafuta suluhu ya kudumu kwenye ishu ya tatizo la wanafunzi shule za Msingi na Sekondari kupata ujauzito.
Leo nimekutana na hii story nikajua kwamba kumbe tatizo hili sio la Bongo peke yake, Indonesia wao wameenda mbali zaidi, Jimbo la Java Mbunge mmoja alitoa pendekezo la kuwa na utaratibu wa kuwapima bikira wanafunzi wa kike wanaomaliza shule za Sekondari, ambaye akikutwa hana basi safari yake kimasomo itaishia hapo hatoruhusiwa kuendelea na masomo.
maxresdefault
Ni nchi hiyo hiyo mwaka jana ilitoka ripoti ya utafiti iliyosema kumekuwa na zoezi la kupima bikira askari wa kike na wanajeshi kitu ambacho kilikosolewa na watu wa haki za binadamu.
Viongozi wa dini pia walilaumu hilo japo walisema kuna dalili zote kwamba ishu hiyo imeendelea kufanywa chini chini kwa siri japo Serikali ilisisitiza kwamba haitoruhusu utaratibu huu kuwepo katika nchi hiyo.
image76
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment