ATM, Supermarket, Internet.. Hizi zote unaambiwa ndani ya Magereza China !!
Movie ya Shawshank Redemption
ni moja ya movies ambazo story yake inahuzunisha, jamaa anakamatwa na
kufungwa gerezani kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake lakini kosa hilo
hakulifanya yeye.
Gerezani akampata rafiki ambaye ni
mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha muda mrefu, alikuwa akimsaidia kwa
vitu vingi, baadaye jamaa akaachiliwa huru, alipofika mtaani alijikuta
kwenye wakati mgumu kutokana na mabadiliko makubwa ambayo aliyakuta.
Sasa ili kuepusha mazingira magumu kwa
wafungwa baada ya kumaliza vifungo vyao, Beijing wametengeneza mji mdogo
ndani ya gereza kwa ajili ya wafungwa waliohukumiwa kifungo cha muda
mrefu, miji hiyo ina huduma kama ATM, treni za umeme, huduma za Benki, hii ni kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao kuona namna mambo yanavyoenda uraiani.
Huduma nyingine zilizoko ndani ya magereza hayo ni pamoja na Internet Cafe na supermarkets.
Sababu ya Serikali kuamua hivyo ni
kuwepo kwa matukio ya watu wengi kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya
kutumikia vifungo ya muda mrefu na kukuta uraiani vitu vingi
vimebadilika kutokana na mabadiliko ya maendeleo ambayo huwa yanatokea
kila wakati.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment