Anawapenda wote, anawahitaji wote na akafanya uamuzi huu ili asiwapoteze…
Mwanamke huyo Mlambo amesema
kuwa anaenjoy maisha kwa kuishi na wanaumea hao wawili katika nyumba
moja na hawezi kuishi na mmoja kwa kuwa anawapenda wote wawili na hayuko
tayari kumpoteza hata mmoja.
Mlambo anaishi nyumba moja na jamaa hao Wesley Gora na Fungai Matandaudyi, amesema
anawapenda wote wawili na kila mmoja anampenda kwa sababu
tofauti, anachijitahidi kukifanya ni kuhakikisha hamkosei hata mmoja
wao, wanaishi kwa furaha kwa sababu walikubaliana kuishi maisha hayo kwa
kuheshimiana.
Gora amesema kuwa
mwanzo alikuwa na hasira alipogundua kuwa mke wake alikuwa na uhusiano
na mtu mwingine, baadae aligundua kuwa mwanamke huyo anawapenda wote
wawili, alikubali kuendelea naye.
Matandaudyi amesema walianza mahusiano miezi nane iliyopita alipogundua kua mpenzi wake ana uhusiano na Wesley walikaa na kuzungumza, wakakubaliana mpango wa kuendelea wote pamoja.
Hii unaionaje mtu wangu?
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment