Siku 6 za Bobbi Kristina akiwa ICU, haya ndio majibu ya madaktari…
Mapema mwishoni mwa juma lililopita Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa marehemu mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston alianguka bafuni na kukimbizwa hospitali huku hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya na kutakiwa kukaa chumba cha uangalizi maalumu.
Imeelezwa kuwa hadi sasa hali yake bado ni mbaya na madaktari wanaomuuguza katika hospitali ya Emory University wamepoteza matumaini na sasa wanaiachia familia yake hatma ya maisha yake.
Chanzo cha habari cha karibu kutoka ndani ya familia hiyo kimedai kuwa hatma ya mtoto huyo iko mikononi mwa baba yake ambaye atatoa muamuzi kama atolewe mashine zinazomsaidia kupumua au la licha ya maamuzi hayo kuwa magumu kwake na kutaka aachwe mwishoni mwa juma hili.
Baba wa mtoto huyo Bobby Brown ana imani na kupona kwa mwanawe kwani katika familia yao kuliwahi kuwa na mgonjwa ambaye alikua na hali mbaya kwa muda wa siku nane lakini alipona.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment