Maneno ya Mo Music kuhusu mapokezi ya single zake mbili kwa mashabiki
Mengi yamezungumzwa kwenye mitandao na sehemu mbalimbali kuhusu ujio wa single mbili za msanii Mo Music ‘Almasi na Simama’ kuwa zimefeli yaani hazipo katika nafasi ya juu (chart) kama ilivyokuwa single yake ya kwanza Basi Nenda wengine wakasema mapokezi ni mabaya.
Sasa time hii Mo Music ame amplify na kuyatoa ya moyoni kuhusiana na single hizo mbili; ‘kwanza
siwezi kusema kwamba hazifanyi vizuri kwasababu tangu siku zinatoka
mpokeo ulikuwa ni wa hali ya juu, pili siwezi kusema haijapokelewa
vizuri kwani hata Basi nenda haikujulikana usiku mmoja ilichukua muda
mpaka kuanza kujulikana kwasababu uandishi mzuri si kama nyimbo zingine
uandishi mzuri wa melody na toni zinaenda katika kueleweka kwa muda
kidogo.
Lakini
mbali na hapo nilikuwa katika maandalizi na mitihani, nilikuwa busy na
shule sikuwa na time ya kusema nitilie mkazo kwa hiyo nikimaliza
mitihani nataanza masuala ya kushoot video na mipango ya kuachia single
nyingine’Alisema Mo Music.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment