Mastaa watatu wa soka wanaoongoza kuwa na followers zaidi ya milioni 10 kwenye Instagram…
Mitandao ya kijamii ni moja ya njia ya
mkato kwa mashabiki kuwafikia mastaa wao, mfano tumeona kwenye Instagram
mastaa wakiweka picha, fans wao wanaweka like, comment zao basi
wanaenjoy kutumia mitandao kuwa karibu na watu wao.
Kwa upande wa mastaa wa soka duniani, mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi amesogea kwenye top three ya wachezaji wa soka wenye followers wengi duniani, Messi ana jumla ya followers milioni 10 katika mtandao wa Instagram.
Messi anakuwa mchezaji wa tatu duniani kwa kuwa na followers wengi huku akiongozwa na mshambuliaji mwenzake Neymar aliyefikisha followers milioni 15.2 na nafasi ya pili ikishikwa na mwanasoka bora duniani Cristiano Ronaldo ambaye ana watu milioni 12.2
“leomessi10M muchas gracias a todos (Thank you very much to all)“– @leomessi
Messi aliweka ujumbe huo kwenye ukurasa
wake Instagram pamoja na picha yake akiwa amevaa jezi yenye namba kumi
mgononi na maneno “MESSi 10 MILLONES”.
No comments:
Post a Comment